Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 35:19-28

Zaburi 35:19-28 BHN

Usiwaache maadui hao wabaya wanisimange, hao wanichukiao bure wafurahie mateso yangu. Maneno wasemayo si ya amani, wanazua maneno ya hila dhidi ya wananchi watulivu. Wananishtaki kwa sauti: “Haya! Haya! Tumeona wenyewe uliyotenda!” Lakini wewe Mwenyezi-Mungu waona jambo hilo, usinyamaze, ee Mwenyezi-Mungu, usikae mbali nami. Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu, ukanitetee; uje, ee Mungu wangu, uangalie kisa changu. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, unitetee, ufanye kulingana na uadilifu wako; usiwaache maadui zangu wanisimange. Usiwaache wajisemee: “Tumefanikiwa tulivyotaka!” Au waseme: “Tumemmaliza huyu!” Waache hao wanaofurahia maafa yangu, washindwe wote na kufedheheka. Hao wote wanaojiona wema kuliko mimi, waone haya na kuaibika. Lakini wanaotaka kuona kuwa sina hatia, wapaaze sauti kwa furaha waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni mkuu mno! Hupendezwa na fanaka ya mtumishi wake.” Hapo nami nitatangaza uadilifu wako; nitasema sifa zako mchana kutwa.

Soma Zaburi 35