Zaburi 35:19-28
Zaburi 35:19-28 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Usiwaache wale wanaonisimanga, wale ambao ni adui zangu bila sababu; usiwaache wale ambao ni adui zangu bila sababu wakonyeze jicho kwa hila. Hawazungumzi kwa amani, bali wanatunga mashtaka ya uongo dhidi ya wale wanaoishi kwa utulivu katika nchi. Hunifumbulia vinywa vyao wakisema, “Aha! Aha! Kwa macho yetu wenyewe tumeliona.” Ee BWANA, umeona hili, usiwe kimya. Usiwe mbali nami, Ee BWANA. Amka, inuka unitetee! Unipiganie Mungu wangu na Bwana wangu. Nihukumu kwa haki yako, Ee BWANA Mungu wangu, sawasawa na haki yako; usiwaache wakusimange. Usiwaache wafikiri, “Aha, hili ndilo tulilotaka!” Au waseme, “Tumemmeza.” Wote wanaofurahia dhiki yangu waaibishwe na wachanganyikiwe; hao wanaojiinua dhidi yangu wavikwe aibu na dharau. Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki wapige kelele za shangwe na furaha; hebu waseme siku zote, “BWANA atukuzwe, ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.” Ulimi wangu utanena haki yako na sifa zako mchana kutwa.
Zaburi 35:19-28 Biblia Habari Njema (BHN)
Usiwaache maadui hao wabaya wanisimange, hao wanichukiao bure wafurahie mateso yangu. Maneno wasemayo si ya amani, wanazua maneno ya hila dhidi ya wananchi watulivu. Wananishtaki kwa sauti: “Haya! Haya! Tumeona wenyewe uliyotenda!” Lakini wewe Mwenyezi-Mungu waona jambo hilo, usinyamaze, ee Mwenyezi-Mungu, usikae mbali nami. Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu, ukanitetee; uje, ee Mungu wangu, uangalie kisa changu. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, unitetee, ufanye kulingana na uadilifu wako; usiwaache maadui zangu wanisimange. Usiwaache wajisemee: “Tumefanikiwa tulivyotaka!” Au waseme: “Tumemmaliza huyu!” Waache hao wanaofurahia maafa yangu, washindwe wote na kufedheheka. Hao wote wanaojiona wema kuliko mimi, waone haya na kuaibika. Lakini wanaotaka kuona kuwa sina hatia, wapaaze sauti kwa furaha waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni mkuu mno! Hupendezwa na fanaka ya mtumishi wake.” Hapo nami nitatangaza uadilifu wako; nitasema sifa zako mchana kutwa.
Zaburi 35:19-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Walio adui zangu bure wasinisimange, Wanaonichukia bila sababu wasining'ong'e. Maana hawasemi maneno ya amani, Ila juu ya watulivu wa nchi huwaza hila. Nao wananifumbulia vinywa vyao, Husema, Ewe! Ewe! Jicho letu limeona. Wewe, BWANA, umeona, usinyamaze; Ee Bwana, usiwe mbali nami. Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumu Kwa ajili ya madai yangu, Mungu wangu na Bwana wangu. Unihukumu kwa haki yako, Ee BWANA, Mungu wangu, Na usiwaache wanisimange. Wasiseme moyoni, Haya! Ndivyo tutakavyo; Wasiseme, Tumemmeza. Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja, Wanaoifurahia hali yangu mbaya. Wavikwe aibu na fedheha, Wanaojikuza juu yangu. Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe BWANA, Apendezwaye na amani ya mtumishi wake. Na ulimi wangu utanena haki yako, Na sifa zako mchana kutwa.
Zaburi 35:19-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Walio adui zangu bure wasinisimange, Wanaonichukia bila sababu wasining’ong’e. Maana hawasemi maneno ya amani, Na juu ya watulivu wa nchi huwaza hila. Nao wananifumbulia vinywa vyao, Husema, Ewe! Ewe! Jicho letu limeona. Wewe, BWANA, umeona, usinyamaze; Ee Bwana, usiwe mbali nami. Uamke, uwe macho ili kunipatia hukumu Kwa ajili ya madai yangu, Mungu wangu na Bwana wangu. Unihukumu kwa haki yako, Ee BWANA, Mungu wangu, Wala wasinisimangize. Wasiseme moyoni, Haya! Ndivyo tutakavyo; Wasiseme, Tumemmeza. Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja, Wanaoifurahia hali yangu mbaya. Wavikwe aibu na fedheha, Wanaojikuza juu yangu. Washangilie na kufurahi, Wapendezwao na haki yangu. Naam, waseme daima, Atukuzwe BWANA, Apendezwaye na amani ya mtumishi wake. Na ulimi wangu utanena haki yako, Na sifa zako mchana kutwa.