Zaburi 5:1-3
Zaburi 5:1-3 BHN
Usikilize maneno yangu, ee Mwenyezi-Mungu, usikie ninavyopiga kite. Usikilize kilio changu, Mfalme wangu na Mungu wangu, maana wewe ndiwe nikuombaye. Ee Mwenyezi-Mungu, alfajiri waisikia sauti yangu, asubuhi nakutolea tambiko yangu, kisha nangojea unijibu.