Wimbo Ulio Bora 7:1-4
Wimbo Ulio Bora 7:1-4 BHN
Nyayo zako katika viatu zapendeza sana! Ewe mwanamwali wa kifalme. Mapaja yako ya mviringo ni kama johari, kazi ya msanii hodari. Kitovu chako ni kama bakuli lisilokosa divai iliyokolezwa. Tumbo lako ni kama lundo la ngano lililozungushiwa yungiyungi kandokando. Matiti yako ni kama paa mapacha, ni kama swala wawili. Shingo yako ni kama mnara wa pembe za ndovu; macho yako ni kama vidimbwi mjini Heshboni, karibu na mlango wa Beth-rabi. Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni, ambao unauelekea mji wa Damasko.