2 Samueli 16:11-12
2 Samueli 16:11-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Tena mfalme Daudi akamwambia Abishai na hata watumishi wake wote, “Ikiwa mtoto wangu mwenyewe anayawinda maisha yangu, je si zaidi mtu wa kabila la Benyamini? Nyinyi mwacheni anilaani kwani Mwenyezi-Mungu amemwagiza anilaani. Huenda Mwenyezi-Mungu akaangalia uovu wangu, naye akanilipa wema kwa laana hii ninayopata leo.”
2 Samueli 16:11-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Daudi akamwambia Abishai, na watumishi wake wote, Angalieni, huyu mwanangu, aliyetoka viunoni mwangu, anautafuta uhai wangu; sembuse Mbenyamini huyu? Mwacheni alaani, kwa sababu BWANA ndiye aliyemwagiza. Labda BWANA atayaangalia mabaya yaliyonipata, naye BWANA atanilipa mema kwa sababu ya kunilaani kwake leo.
2 Samueli 16:11-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Daudi akamwambia Abishai, na watumishi wake wote, Angalieni, huyu mwanangu, aliyetoka viunoni mwangu, anautafuta uhai wangu; si zaidi Mbenyamini huyu sasa? Mwacheni alaani, kwa sababu BWANA ndiye aliyemwagiza. Labda BWANA atayaangalia mabaya yaliyonipata, naye BWANA atanilipa mema kwa sababu ya kunilaani kwake leo.
2 Samueli 16:11-12 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo Daudi akamwambia Abishai na maafisa wake wote, “Mwanangu, yeye ambaye ametoka viunoni mwangu mwenyewe, anajaribu kuuondoa uhai wangu. Je, si zaidi sana kwa huyu Mbenyamini! Mwacheni, acha alaani, kwa maana BWANA amemwambia afanye hivyo. Inawezekana kwamba BWANA ataona dhiki yangu na kunilipa mema kwa ajili ya laana ninayopokea leo.”