Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 46:16-24

Ezekieli 46:16-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Bwana MUNGU asema hivi; Mkuu akimpa mwanawe awaye yote zawadi, ni urithi wake, itakuwa mali ya wanawe; ni milki yao kwa kurithiwa. Bali akimpa mmoja wa watumishi wake baadhi ya urithi wake, itakuwa mali yake mpaka mwaka wa kuacha huru; ndipo itakapomrudia mkuu; lakini urithi wake, huo utakuwa wa wanawe. Tena mkuu hatawaondolea watu urithi wao, hata kuwatoa kwa nguvu katika milki yao; atawapa wanawe urithi katika mali yake mwenyewe, watu wangu wasije wakatawanyika, kila mtu mbali na milki yake. Ndipo akanileta kati ya maingilio, yaliyokuwa kando ya lango, mpaka vyumba vitakatifu vya makuhani, vilivyoelekea upande wa kaskazini; na tazama, palikuwa na mahali, upande wa nyuma ulioelekea magharibi. Akaniambia, Hapa ndipo mahali pa makuhani, watakapoitokosa sadaka ya hatia, na sadaka ya dhambi, watakapoioka sadaka ya unga; kusudi wasizilete nje katika ua wa nje, na kuwatakasa watu. Kisha akanileta mpaka ua wa nje, akanipitisha karibu na pembe nne za ua huo; na tazama, katika kila pembe ya ua huo palikuwa na kiwanja. Katika pembe nne za ua huo palikuwa na viwanja vilivyoungana, urefu wake dhiraa arobaini, na upana wake thelathini; viwanja hivyo vinne vya pembeni vilikuwa vya kipimo kimoja. Tena palikuwa na safu ndani yake pande zote, kuvizunguka vile viwanja vinne; tena palifanywa meko ya kutokosea, chini ya safu pande zote. Ndipo akaniambia, Hizi ni nyumba za kutokosea, ambamo wahudumu wa nyumba watatokosa sadaka za watu.

Ezekieli 46:16-24 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

“ ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Ikiwa mkuu atawalaye atatoa zawadi kutoka kwenye urithi wake na kumpa mmoja wa wanawe, hiyo zawadi itakuwa pia kwa wazao wake, itakuwa mali yao kwa urithi. Hata hivyo, kama atatoa zawadi kutoka urithi wake na kumpa mmoja wa watumishi wake, mtumishi anaweza kuiweka mpaka mwaka wa uhuru, kisha itarudishwa kwa mkuu anayetawala. Urithi wake ni wa wanawe peke yao, ni mali yao. Mkuu anayetawala hana ruhusa kuchukua urithi wowote wa watu na kuwaondoa kwenye mali zao. Mkuu atawalaye atawapa wanawe urithi wao, kutoka kwenye mali zake mwenyewe, ili kwamba pasiwe na mtu wangu yeyote atakayetengwa na urithi wake.’ ” Kisha mtu yule akanileta kwa kupitia kwenye ingilio lililokuwa kando ya lango mpaka kwenye vyumba vitakatifu vinavyoelekea kaskazini, ambavyo ni vya makuhani, naye akanionyesha mahali fulani upande wa mwisho wa magharibi. Akaniambia, “Mahali hapa ndipo makuhani watakapotokosea sadaka ya hatia na sadaka ya dhambi na kuoka sadaka ya nafaka, kuepuka kuzileta katika ukumbi wa nje na kushirikisha utakatifu kwa watu.” Baada ya hapo akanileta kwenye ukumbi wa nje na kunizungusha kwenye pembe zake nne, nami nikaona katika kila pembe ya huo ukumbi kulikuwa na ukumbi mwingine. Katika pembe nne za huo ukumbi wa nje kulikuwa na kumbi nyingine, zenye urefu wa dhiraa arobaini na upana wake dhiraa thelathini, ambapo hizo kumbi kwenye hizo pembe nne zilikuwa na vipimo vilivyo sawa. Mzunguko wa ndani wa hizo kumbi nne ulikuwa na ukingo wa jiwe, zikiwa na sehemu zilizojengwa kwa ajili ya moto kuzunguka chini ya huo ukingo. Akaniambia, “Hizi ndizo sehemu za kupikia ambazo wale wanaohudumu kwenye Hekalu watatokosea dhabihu za watu.”

Ezekieli 46:16-24 Biblia Habari Njema (BHN)

“Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Ikiwa mtawala anampa mmojawapo wa wanawe zawadi ya ardhi, zawadi hiyo itakuwa mali ya huyo kijana milele kama sehemu ya jamaa yake. Lakini ikiwa atampa mmoja wa watumishi wake sehemu yoyote ya ardhi yake, zawadi hiyo itakuwa mali yake mpaka mwaka wa kuachwa huru. Ndipo itakapomrudia mtawala. Ni yeye tu na watoto wake wa kiume wanaoweza kuimiliki daima. Mtawala kamwe asipore mali ya watu. Ardhi yoyote anayowapa watoto wake wa kiume ni lazima itokane na eneo lake mwenyewe. Hivyo hatawadhulumu watu wangu kwa kuwanyanganya ardhi yao.” Kisha, yule mtu akanipitisha kwenye nafasi ya kupitia kuingia kwenye vyumba vitakatifu vya makuhani vinavyoelekea kaskazini, karibu na lango la kusini la ukumbi wa ndani. Akanionesha mahali, upande wa magharibi wa vyumba, akaniambia: “Hapa makuhani huchemsha nyama ya sadaka ya kuondoa hatia, sadaka ya kuondoa dhambi, na kuoka sadaka za nafaka. Kwa hiyo hawatoki nje ya ukumbi na chochote, ili watu wasije wakawa najisi kwa kugusa kitu kitakatifu.” Kisha akanipeleka kwenye uwanja wa nje, akanipitisha karibu na pembe nne za ua; kwa kila pembe ya ua kulikuwapo kiwanja kidogo, yaani, kwa pembe nne za ua vilikuwapo viwanja vinne vidogo vya urefu wa mita 20 na upana mita 15. Ulikuwapo ukuta kukizunguka kila kiwanja, na mahali pa moto mkabala na ukuta. Yule mtu akaniambia: “Haya ni majiko ambako watumishi wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu watachemsha sadaka wanazoleta watu.”

Ezekieli 46:16-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Bwana MUNGU asema hivi; Mkuu akimpa mwanawe awaye yote zawadi, ni urithi wake, itakuwa mali ya wanawe; ni milki yao ya kurithiwa. Bali akimpa mmoja wa watumishi wake baadhi ya urithi wake, itakuwa mali yake mpaka mwaka wa kuacha huru; ndipo itakapomrudia mkuu; lakini urithi wake, huo utakuwa wa wanawe. Tena mkuu hatawaondolea watu urithi wao, hata kuwatoa kwa nguvu katika milki yao; atawapa wanawe urithi katika mali yake mwenyewe, watu wangu wasije wakatawanyika, kila mtu mbali na milki yake. Ndipo akanileta kati ya maingilio, yaliyokuwa kando ya lango, mpaka katika vyumba vitakatifu vya makuhani, vilivyoelekea upande wa kaskazini; na tazama, palikuwa na mahali, upande wa nyuma ulioelekea magharibi. Akaniambia, Hapa ndipo mahali pa makuhani, watakapoitokosa sadaka ya hatia, na sadaka ya dhambi, watakapoioka sadaka ya unga; kusudi wasizilete nje katika ua wa nje, na kuwatakasa watu. Kisha akanileta mpaka ua wa nje, akanipitisha karibu na pembe nne za ua huo; na tazama, katika kila pembe ya ua huo palikuwa na kiwanja. Katika pembe nne za ua huo palikuwa na viwanja vilivyoungana, urefu wake dhiraa arubaini, na upana wake thelathini; viwanja hivyo vinne vya pembeni vilikuwa vya kipimo kimoja. Tena palikuwa na safu ndani yake pande zote, kuvizunguka vile viwanja vinne; tena palifanywa meko ya kutokosea, chini ya safu pande zote. Ndipo akaniambia, Hizi ni nyumba za kutokosea, ambamo wahudumu wa nyumba watatokosa sadaka za watu.