Isaya 63:1
Isaya 63:1 Biblia Habari Njema (BHN)
Ni nani huyu ajaye kutoka Edomu, anayefika kutoka Bosra na mavazi ya madoa mekundu? Ni nani huyo aliyevaa mavazi ya fahari, anatembea kwa nguvu zake kubwa? Ni mimi Mwenyezi-Mungu ninayetangaza ushindi wangu; nami ni mwenye nguvu ya kuokoa.
Isaya 63:1 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ni nani huyu atokaye Edomu, Atokaye Bosra akiwa na mavazi yenye madoa mekundu? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Ndimi nisemaye kwa haki, Niliye hodari wa kuokoa.
Isaya 63:1 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ni nani huyu atokaye Edomu, Mwenye mavazi ya kutiwa damu kutoka Bosra? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Mimi nisemaye kwa haki, Hodari wa kuokoa.
Isaya 63:1 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ni nani huyu anayekuja kutoka Edomu, kutoka Bosra, mwenye mavazi yaliyotiwa madoa mekundu? Ni nani huyu, aliyevikwa joho la kifahari, anayetembea kwa ukuu wa nguvu zake? “Mimi ndimi, nisemaye katika haki, mwenye nguvu wa kuokoa.”