Yobu 11:13-15
Yobu 11:13-15 Biblia Habari Njema (BHN)
“Yobu, ukiufanya moyo wako mnyofu, utainua mikono yako kumwomba Mungu! Kama una uovu, utupilie mbali. Usikubali ubaya uwemo nyumbani mwako. Hapo utajitokeza mbele ya watu bila lawama, utakuwa thabiti bila kuwa na hofu.
Yobu 11:13-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wewe ukiuweka moyo wako kwa uelekevu, Na kumnyoshea mikono yako; Ikiwa una uovu mkononi mwako, uweke mbali nawe, Wala usikubali upuzi kukaa hemani mwako; Hakika ndipo utakapopata kuinua uso pasipo ila; Naam, utathibitika, wala hutakuwa na hofu
Yobu 11:13-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Hata sasa ukiutoa moyo wako kwake na kumwinulia mikono yako, ukiiondolea mbali ile dhambi iliyo mkononi mwako wala usiuruhusu uovu ukae hemani mwako, ndipo utainua uso wako bila aibu; utasimama imara bila hofu.
Yobu 11:13-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)