Yobu 9:22-24
Yobu 9:22-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Yote ni mamoja, kwa hiyo nasema; Mungu huwaangamiza wema na waovu. Maafa yaletapo kifo cha ghafla, huchekelea balaa la wasio na hatia. Nchi ikitiwa watu waovu katika utawala wa mwovu, Mungu huyafumba macho ya mahakimu wake! Kama si yeye afanyaye hivyo, ni nani basi?
Yobu 9:22-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hayo yote ni mamoja; kwa hiyo nasema, Yeye huangamiza wakamilifu na waovu pia. Kama hilo pigo likiua ghafla, Atayadhihaki majaribu yake asiye na kosa. Dunia imetiwa mkononi mwa waovu; Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake; Kama si yeye, ni nani basi?
Yobu 9:22-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hayo yote ni mamoja; kwa hiyo nasema, Yeye huangamiza wakamilifu na waovu pia. Kama hilo pigo likiua ghafula, Atayadhihaki majaribu yake asiye na kosa. Dunia imetiwa mkononi mwa waovu; Yeye hufunika nyuso za waamuzi wake; Kama si yeye, ni nani basi?
Yobu 9:22-24 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Hayo yote ni sawa; ndiyo sababu nasema, ‘Yeye huwaangamiza wasio na makosa pamoja na waovu.’ Wakati wa pigo liletapo kifo cha ghafula, yeye hudhihaki kule kukata tamaa kwa yule asiye na kosa. Nchi inapoangukia mikononi mwa waovu, yeye huwafunga macho mahakimu wake. Kama si yeye, basi ni nani?