Ufunuo 11:18
Ufunuo 11:18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumishi wako manabii na watakatifu, na hao walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi.
Ufunuo 11:18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na mataifa walikasirika, hasira yako nayo ikaja, na wakati ukaja wa kuhukumiwa waliokufa, na wa kuwapa thawabu yao watumwa wako manabii na watakatifu, na hao walichao jina lako, wadogo kwa wakubwa, na wa kuwaharibu hao waiharibuo nchi.
Ufunuo 11:18 Biblia Habari Njema (BHN)
Watu wa mataifa waliwaka hasira, lakini ghadhabu yako imefika, naam wakati wa kuwahukumu wafu. Ndio wakati wa kuwatuza watumishi wako manabii, watakatifu na wote wanaolitukuza jina lako, wakubwa kwa wadogo. Ni wakati wa kuwaangamiza waangamizi wa dunia.”
Ufunuo 11:18 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mataifa walikasirika nao wakati wa ghadhabu yako umewadia. Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa na kuwapa thawabu watumishi wako manabii na watakatifu wako pamoja na wale wote wanaoliheshimu Jina lako, wakubwa kwa wadogo: na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”