Ufunuo 7:3-4
Ufunuo 7:3-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Msiidhuru nchi wala bahari, wala miti, hadi tuwe tumetia muhuri kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu wetu.” Ndipo nikasikia idadi ya wale waliotiwa muhuri: yaani 144,000 kutoka makabila yote ya Israeli.
Ufunuo 7:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
“Msiharibu nchi, wala bahari, wala miti, mpaka tutakapokwisha wapiga mhuri watumishi wa Mungu wetu katika paji la uso.” Kisha, nikasikia idadi ya hao waliopigwa mhuri: Watu 144,000 wa makabila yote ya watu wa Israeli.
Ufunuo 7:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hadi tutakapokwisha kuwatia mhuri watumishi wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Nikasikia hesabu yao waliotiwa mhuri katika kila kabila la Waisraeli, watu elfu mia moja na arubaini na nne.
Ufunuo 7:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.