Soma Biblia Kila Siku 2Mfano

Ingawa Musa alilelewa nyumbani kwa Farao, alikuwa anafahamu asili yake mwenyewe. Musa ni mtu wa haki, lakini katika ujana wake alitenda matendo kwa haraka mno bila kuyafikiria sana. "Mshahara" wa majaribio yake ya kutenda haki na kuwapigania ndugu zake ulikuwa kwamba alilazimika kukimbia chuki ya Farao. Alikimbilia nchi ya Midiani. Badala ya kuwa mtu ajulikanaye huko Misri, akawa ni mtu asiyejulikana hapo Midiani. Alikuwa mkimbizi tu. Inaonekana kana kwamba ameachwa na Mungu, lakini kesho tutaona kwamba sivyo ilivyo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 2 inakupa mpango wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu, hasa kutoka Kitabu cha Kutoka na Injili ya Yohana, pamoja na maelezo juu ya somo hilo.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz