Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yesu: Bendera Wetu wa UshindiMfano

Jesus: Our Banner of Victory

SIKU 5 YA 7

Ushindi dhidi ya Magonjwa

Neno la Mungu linatuambia kwamba kwa kuoigwa kwake Yesu tumepona. Yesu alipokufa na kufufuka tena, alishinda dhambi, mauti na magonjwa katika hali zote milele. Inashangaza kwamba, kupitia kwake, tunashiriki ushindi huu! Lakini ushindi dhidi ya magonjwa una maana gani kwetu wakati bado tunaishi katika ulimwengu ulioanguka?

Kwenye Agano Jipya lote, tunaona mifano ya uponyaji wa ajabu alioufanya Yesu pamoja na mitume wakifanya kupitia nguvu ya jina lake. Katika kusoma shuhuda hizi za uponyaji, ni rahisi kufikiria kwamba Mungu atajibu maombi yetu kuhusu magonjwa kwa njia fulani: Kupona maumivu mara moja, kupona mara moja ugonjwa usiopona au ushindi kamili kutokana na wasiwasi. Kwa hiyo tunafanyaje tunapoona uzoefu wetu hauendani na matarajio yetu? Tunatakiwa kuwa makini ili tusiathiri jinsi uponyaji ulivyo.

Mtume Paulo anatueleza katika Warumi 8:28 kwamba Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao. Hilo halimaanishi kila linalotokea ni jema- ushindi wa Yesu dhidi ya dhambi na mauti haukuondoa majaribu yote katika maisha yetu duniani. Ukweli, katika Yohana 16:33, Yesu aliahidi kwamba kwamba tutapata dhiki, na magonjwa kama sehemu ya dhiki tutakazokabiliana nazo. Wakati Mungu anaingilia kati mara nyingi kwa njia za miujiza, hatujahakikishiwa uponyaji kamili upande huu wa mbingu. Lakini tunaweza kuwa na uhakika wak ushindi wa milele ambao wokovu wetu unatuhakikishia. Tunakuwa milelel katika uwepo wa Mungu, wenye furaha na mbali na magonjwa, dhambi, mauti, maumivu na wasiwasi.

Usivunjike moyo kwa kile kinachoonekana kama maombi yasiyojibiwa au matokeo ambayo hayako kama ulivyotarajia. Mungu husikia maombi yetu, na katika mambo yote, hufanya mema kwa ajili yako na utukufu wake. Tunapoendelea na majira haya ya Pasaka, mwombe Mungu akupe ufahamu wa milele. Tunapoweka uhalisia wa Mbinguni akilini mwetu, tunaweza kuomba kwa ujasiri na kutembea kwa ujasiri katika kila jaribu tukijua kwamba hata iweje, tunashinda.

Download today's image here

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Jesus: Our Banner of Victory

Tunapo sherehekea Pasaka, tunasherehekea ushindi mkuu katika historia. Kupitia kifo cha Yesu na kufufuka, alishinda nguvu ya dhambi na kaburi, na athari zake zote, na alichagua kushiriki ushindi huo nasi. Pasaka hii, hebu tuangalie baadhi ya ngome alizozishinda, angalia vita alivyovipiga kwa ajili yetu, na umsifu kama bendera ya ushindi wetu.

More

Tungependa kushukuru Church of the Highlands kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.churchofthehighlands.com