Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yesu: Bendera Wetu wa UshindiMfano

Jesus: Our Banner of Victory

SIKU 6 YA 7

Ushindi dhidi ya majaribu

Hatuhitaji mtu atukumbushe kuwa majaribu ni halisi --haujawahi kutokea ulimwengu kuwa na ufahamu kiasi hiki cha kubofya kifungo tuu unajua kila kitu. Lakini je, tumewahi kuacha kufikiria njia mbali mbali ambazo shetani anajaribu kutujaribu? Tunahitaji kujua majaribu yanafanyaje kazi, ili tuweze kujilinda vyema dhidi ya majaribu hayo.

Katika Mwanzo, shetani alimjaribu Hawa kwa kuhoji neno la Mungu na Makusudi yake, na kukubali kwake kukaleta dhambi na mauti ulimwenguni. Katika 2 Samweli, mfalme Daudi alichagua kukaa nyumbani wakati " wafalme wanatoka kwenda vitani," akiwatuma wengine kupigana kwa niaba yake. Kama Daudi angekuwa mahali Mungu alipomwita kuwepo, kamwe asingekuwa peke yake juu ya paa akimwangalia Batisheba. Matokeo yake, tunaona uzinzi na mauaji yakiingia kwenye habari ya Daudi. Na wakati Roho alipomwongoza Yesu kwenye nyikani katika Mathayo 4, shetani alijaribu kumjaribu Mwana wa Mungu kwa kunukuu maandiko.

Adui siku zote anajitahidi kutufanya tuhoji neno la Mungu, mpango wake, na moyo wake kwetu. Kama shetani anaweza kututega katika mazungumzo haya, ni mteremko wenye utelezi utakaoleta vurugu na maumivu kwenye maisha yetu. Lakini Yesu anajua jinsi ilivyo jaribu la kumhoji Mungu- ukweli ni, kwamba amepitia majaribu haya- na amefanya njia kukataa kila jaribu tunalopitia - na kutembea katika uhuru. Wakati Yesu alipolipa deni letu la dhambi msalabani, hatuko tena chini ya mamlaka ya shetani!

Ni muhimu kukumbuka kwamba kutembea katika ushindi wa Yesu dhidi ya majaribu inabeba makusudi makubwa katika upande wetu. Tunahitaji kukiri kila siku kwamba adui atajaribu kila siku kuturudisha katika himaya yake maishani mwetu na tunahitaji kuwa macho, kujenga ulinzi kuyalinda maisha yetu ya uhuru katika Yesu, tukimwomba Mungu msaada wa kikabiliana na majaribu, na kuzungukwa na marafiki wamjuao Mungu watakaotuwajibisha. Mtume Paulo alisema katika Waefeso 6 kwamba tunahitaji kuvaa silaha zote za Mungu ili tuweze kuzipinga hila za shetani.

Tunapoendelea na juma hili la Pasaka, kumbuka kwamba Yesu amemvua adui nguvu juu yako. Omba pamoja na. Waefeso 6: 10-18 na kuvaa silaha zake kila siku. Mshukuru Mungu kwa kupa nguvu kuishi katika uhuru dhidi ya majaribu, na umwombe Mungu kama kuna eneo ambalo kiwango cha umakini wako unahitaji kuongezeka. Utakusaidia kutambua mahali ulipo dhaifu na kukupa nguvu kusimama kinyume na adui. Katika ushindi wa Yesu, hutashindwa!

Download today's image here

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Jesus: Our Banner of Victory

Tunapo sherehekea Pasaka, tunasherehekea ushindi mkuu katika historia. Kupitia kifo cha Yesu na kufufuka, alishinda nguvu ya dhambi na kaburi, na athari zake zote, na alichagua kushiriki ushindi huo nasi. Pasaka hii, hebu tuangalie baadhi ya ngome alizozishinda, angalia vita alivyovipiga kwa ajili yetu, na umsifu kama bendera ya ushindi wetu.

More

Tungependa kushukuru Church of the Highlands kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: https://www.churchofthehighlands.com