Soma Biblia Kila Siku 7Mfano
Maono anayokutana nayo Danieli yanamtisha. Hata anakuwa bubu na kuishiwa nguvu mpaka “mmoja mfano wa mwanadamu” anapomgusa na kuongea naye. Tufikiri juu ya Yesu hapo. Anapoongea nasi, hapo ndipo kuna kutiwa nguvu (m.19: Akasema, Ee mtu upendwaye sana, usiogope; amani na iwe kwako, uwe na nguvu, naam, uwe na nguvu. Aliposema nami nikapata nguvu, nikasema, Ee Bwana wangu, na aseme Bwana wangu; kwa maana umenitia nguvu). Kwa hiyo umsikilize daima. Ndivyo Mungu anavyoleta uponyaji unapoumizwa, amani unaposumbuka, na nguvu uwapo dhaifu. Danieli anasaidiwa kujua vita kali iliyopo kati ya wema na uovu. Uombapo, uovu hupinga maombi, lakini hali ya leo na ya baadaye iko mikononi mwa Mungu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 7 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kuelewa zaidi.
More
Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz