Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SABAMfano

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SABA

SIKU 4 YA 7

  

KULISHA WATU ELEFU TANO

1 Baada ya haya, Yesu alikwenda ng'ambo ya Bahari ya Galilaya, ambayo pia huitwa Bahari ya Tiberia.

2 Umati mkubwa wa watu uliendelea kumfuata, kwa sababu waliona ishara nyingi za miujiza alizofanya kwa wagonjwa."

3 Kisha Yesu akapanda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake.

4 Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia."

5 Yesu alipotazama na kuuona ule umati mkubwa wa watu ukimjia, akamwambia Filipo,

“Tutanunua wapi mikate ili watu hawa wale?”

6 Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya.

7 Filipo akamjibu, “Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili, hazitoshi kununua mikate ya kuwapa watu hawa kila mtu apate kidogo.”

8 Mmoja wa wanafunzi wake, aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akamwambia,

9 “Hapa kuna mvulana mmoja mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo. Lakini hivi vitatosha nini kwa umati wote huu?”

10 Yesu akasema, “waketisheni watu chini.”

Palikuwa na majani mengi katika eneo lile, nao watu wakaketi, palikuwa na wanaume 5,000.

11 Ndipo Yesu akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu na kuwagawia wale watu waliokuwa wamekaa kwa kiasi walichohitaji. Akafanya vivyo hivyo na wale samaki. Kila mtu akapata kadiri alivyotaka.

12 Watu wote walipokwisha kula na kushiba, akawaambia wanafunzi wake,

“Kusanyeni vipande vilivyobaki vya ile mikate, kisipotee cho chote.”

13 Hivyo wakavikusanya wakajaza vikapu kumi na viwili kwa vipande vilivyobaki vya ile mikate mitano na samaki wale wawili wadogo.

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SABA

Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana

More

Tunapenda kushukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org