INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SABAMfano
![INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SABA](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F15976%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
KULISHA WATU ELEFU NNE
Katika siku hizo, umati mkubwa wa watu ulikusanyika tena. Kwa kuwa walikuwa hawana chakula, Yesu akawaita wanafunzi wake akawaambia,
2 “Ninauhurumia huu umati wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu na hawana chakula.Nikiwaaga waende nyumbani bila kula, watazimia njiani kwa sababu baadhi yao wametoka mbali.”
4 Wanafunzi wake wakamjibu,
“Lakini hapa nyikani tutapata wapi mikate ya kutosha kuwalisha?”
5 Yesu akawauliza,“Mna mikate mingapi?” Wakajibu, “Tuna mikate saba.”
6 Akawaambia watu waketi chini.
Akiisha kuichukua mikate saba na kushukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi wake ili wawagawie watu.
Wanafunzi wake wakafanya hivyo.Walikuwa pia na visamaki vichache, Yesu akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu. Wale watu walikula na kutosheka,
baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia wakajaza vikapu saba.Watu waliokula walikuwa wapata 4,000. Akiisha kuwaaga,
10 aliingia kwenye mashua pamoja na wanafunzi wake akaenda sehemu za Dalmanutha.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![INJILI ULIMWENGUNI - SEHEMU YA SABA](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F15976%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Mfuatano huu ni kusanyiko la hadithi kuhusu maisha Kristo itakayoshirikisha watazamaji wote ulimwenguni kwa kutumia mchanganyiko wa kuona na sauti. Maisha na mafundisho ya Yesu yalidhihirishwa katika kitabu hiki cha hadithi ambacho kinafuata masimulizi ya Agano Jipya yanayopatikana katika vitabu vya Injili vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
More
Tunapenda kushukuru GNPI Afrika kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://gnpi-africa.org