Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 8Mfano

Soma Biblia Kila Siku 8

SIKU 12 YA 31

BWANA atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia (m.64). Mungu anatabiri jinsi atakavyolitawanya taifa la Israeli. Ndivyo ilivyotokea hasa mwaka 586 kK walipopelekwa Babeli. Wachache wakarudi baadaye. Uhamisho mwingine mkubwa ni mwaka 70 bK. Wakati huo serikali ya Rumi ilitawala humo Israeli, na iliwaondoa Wayahudi wengi mno. Wakaendelea kutawanyika hadi mabara yote ya dunia. Mara kwa mara Wayahudi wameteswa na kuudhiwa sana katika nchi mbalimbali (m.65-67: Katika mataifa hayo hutapata raha iwayo yote, wala hutakuwa na kituo cha wayo wa mguu wako; lakini Bwana atakupa huko moyo wa kutetema, na macho ya kuzimia, na roho ya kudhoofika; na uzima wako utakuwa na wasiwasi mbele yako; nawe utakuwa na woga usiku na mchana, wala hutaamini kamwe maisha yako; asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona).

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 8

Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz