Soma Biblia Kila Siku 8Mfano
Nyakati za Musa, mtoaji wa agano akishafunua masharti yake n.k. ndani ya agano hilo, alikuwa anawawekea watu wahusika laana na baraka kufuatana na watakavyolifuata hilo agano. Ndivyo Mungu anavyofanya hapa. Anawawekea Waisraeli laana na baraka pamoja na mauti na uzima, sambamba na jinsi watakavyolifuata Neno lake. Katika somo hili tunasikia laana itakayowaangukia kama wasipofanya hivyo. Je, watapuuza au kuzingatia kwamba Yeye pekee ategemewe na kuabudiwa nao? Waitike Aminakuwa wameikubali laana ya Mungu inayosema, Alaaniwe asiyeyaweka maneno ya torati hii kwa kuyafanya (m.26). Linganisha na Gal 3:10 inayosema, Wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati, ayafanye.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz