Soma Biblia Kila Siku 8Mfano
Laana zinagusa maisha mazima ya kilimo, ufugaji, ndoa, uchumi, afya n.k. Tena Waisraeli wanatangaziwa kuwa Mungu atawafukuza kutoka katika nchi ya Kaanani na kuwapeleka kwa taifa lingine ambapo watakuwa ushangao, na mithali, na dharau kwa watu wengine(m.36-37). Ndivyo ilivyotokea miaka mingi baadaye Wayahudi walipochukuliwa mateka kwenda Ashuru na Babeli: Mfalme wa Babeli akamchukua mateka [Yekonia, mfalme wa Yuda] katika mwaka wa nane wa kutawala kwake. Akatoa huko hazina zote za nyumba ya Bwana, na hazina za nyumba ya mfalme ... Akawachukua mateka watu wa Yerusalemu wote pia, na wakuu wote, na mashujaa wote, watu elfu kumi; na mafundi wote, na wafua chuma wote; hapana mtu aliyebaki, ila waliokuwa wanyonge wa watu wa nchi(2 Fal 24:12-14). Ndugu, tusimchezee na kumdharau Mungu kwa kujidai kuwa tuko chini ya baraka tu wakati tunaitegemea miungu. Si kweli!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 8 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku hasa katika kitabu cha Matendo ya Mitume, Kumbukumbu la Torati, na Yohana pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz