Soma Biblia Kila Siku 9Mfano
Akili haikubali wokovu wa bure namna hii! Je, Ibrahimu hakufanya tendo lolote ili apewe uheri huu? Huenda alikuwa ametahiriwa kwanza, na halafuimani yake ikahesabiwa kuwa ni haki?! Hapana, hapana! Ibrahimu alihesabiwaje basi? Alipokwisha kutahiriwa, au kabla hajatahiriwa? Si baada ya kutahiriwa, bali kabla ya kutahiriwa(m.10). Neema ni neema. Humo hakuna madai yoyote. Kutahiriwa kwa Ibrahimu kulifuata baadaye kama alama ya kuthibitisha kuwa alikwisha hesabiwa haki kwa imani (m.11: Aliipokea dalili hii ya kutahiriwa, muhuri ya ile haki ya imani aliyokuwa nayo kabla hajatahiriwa). Kwa hiyo kwa mtu aliyetahiriwa na mtu asiyetahiriwa hali ni hii moja: Wote wanahesabiwa haki bure kwa kuamini neema ya Mungu iliyofunuliwa katika Yesu Kristo!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz