Soma Biblia Kila Siku 12Mfano
Roho ya kuasi imekuwapo tangu alipoishi Paulo (m.7: Ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi). Lakini bado yule mwovu hajafunuliwa (m.8: Ndipo atakapofunuliwa yule asi). Hajafunulia kwa sababu bado si wakati wake (m.6: Na sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake). Yaani ni Mungu anayemzuia. Lizuialo au azuiaye (m.6n), huenda maana yake ni jamii iliyojengwa juu ya haki, watu kujali amri za Mungu, au ushirika wa waumini. Ingawa yule asi atakuja kwa uwezo wote wa Shetani (m.9:Kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo), hatamweza Yesu atakapofunuliwa (m.8: Yule asi … Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake). Angalia kwamba kutokea kwa mpinga Kristo ni mwanzo wa hukumu ya Mungu juu ya wasioiamini kweli ya Injili (m.10-12: Kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa … kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu). Lakini kipindi hichohicho waumini wataokolewa. Angalia uhakika wa Paulo. Hata hapo anapoandika anaweza kumshukuru Mungu kwa ajili ya kuokoka kwao! Imetupasa sisi kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, ndugu mliopendwa na Bwana, kwa kuwa Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli; aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo(2:13).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wathesalonike na Zaburi.
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz