Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12

SIKU 21 YA 31

Kabla Yesu hajaja, waumini huhitaji faraja na maonyo juu ya kusimama imara katika imani (ni maonyo hayo yaliyoandikwa katika 2:13-3:15). Imani isiyolegea yawezekana tu tunapolishika Neno la Mungu, tukikubali kuipenda ile kweli. Maana kwa njia hiyo Mungu hutuita tuwe watu wake (m.14: Aliwaitia ninyi kwa injili), hututakasa (m.13: Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho. Hulingana na Yesu alivyoomba katika Yn 17:17, Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli), hutupa tumaini jema, na kutufariji (m.16-17: Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema, awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema). Hivyo tutaimarika kiimani, na maisha yetu yote ya kila siku yatashuhudia neema na wema wake Mungu. Tafakari pia aya hizi zinavyomshuhudia Paulo. Ndiye mfano mzuri wa neno katika 1 The 5:17 linalosema, Ombeni bila kukoma.

siku 20siku 22

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12

Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wathesalonike na Zaburi.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz