Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12

SIKU 4 YA 31

Shemu, na Hamu, na Yafethi … Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu; na kwa hao nchi yote ikaenea watu (m.18-19). Yaani duniani pote walibaki hao tu! Ndiyo maana Mungu akawaambia: Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi (9:7)! Yaani, mataifa yote yana asili yao kwa wana wa Nuhu. Sura ya 10 inaeleza juu ya ukoo wao. Hapa twaona k.m. asili ya watu wa Ulaya ni kwa Yafethi, Wamisri na Waethiopia wametoka kwa Hamu na Waisraeli na Waarabu wametoka kwa Shemu. Kuhusu hao wote, Yesu anasema, Habari njema ya ufalme itahubiriwa kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja(Mt 24:14).

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12

Soma Biblia Kila Siku 12 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kitabu cha Mwanzo, Mathayo, 2 Wathesalonike na Zaburi.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana