Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/20Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/20

SIKU 24 YA 29

Kuwa Mkristo wa kweli au kuwa mtumishi wa kanisa uliyetumwa kwa watu, mara nyingi kumekuwa na ugumu wake. Hali hii Yesu hutuambia wazi. Watu wengi hawataki kusikia ukweli, na wanataka wewe usiufuate ukweli. Giza linachukia nuru. Hapo panahitajika uvumilivu! Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu; lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka(m.22). Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka(Yn 15:18-21). Lakini Yesu pia hutupatia faraja. Katika mambo yote tuko chini ya uongozi wake na hata tukikutana na mambo magumu sana hatutakosa kuona uwepo wake! Tena atatuwezesha kumshuhudia hata katika hali hiyo ngumu. Rudia kusoma m.17-20.

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/20

Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana