Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 02/20Mfano

Soma Biblia Kila Siku 02/20

SIKU 28 YA 29

Mungu anajua mambo yetu yote: tunayofanya, tunayofikiri, tunakokwenda na tunayosema. Kwa Mkristo jambo hili linamletea usalama. Hakuna mahali ambapo Mungu hayupo. Mungu yupo pamoja naye (m.9-10: Ningezitwaa mbawa za asubuhi, Na kukaa pande za mwisho za bahari; Huko nako mkono wako utaniongoza, Na mkono wako wa kuume utanishika). Kwa mtu anayemkataa Mungu jambo hilo linamletea shida, kwa sababu anapojaribu kutafuta njia ya kutoroka kutoka kwa Mungu mwenye nguvu namna hiyo, anagundua kwamba binadamu hawezi kumtoroka Mungu awezaye kwenda mahali po pote. Giza na nuru ni sawa machoni pa Mungu anayemwona daima.

siku 27siku 29

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 02/20

Soma Biblia Kila Siku 02/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Esta. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu.

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

Mipango inayo husiana