Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Lile lillilokuwako tangu mwanzo ... habari ya Neno la uzima (m.1). Neno la uzima ni neno lenye uhai ndani yake: Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima (Yn 1:4a; ling. Yn 14:6 Yesu anaposema, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima). Neno la uzima lililokuwako tangu mwanzo lilileta uhai kwa yote (Yn 1:1 na 3,Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. … Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika). Yaani, Neno lilikuwako kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu. Mwanafunzi wa Yesu alilisikia, aliliona na alilipapasa kwa sababu uzima ulidhihirika kwetu katika Yesu Kristo (m.2,Uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu). Lengo ni kuitimiza furaha yetu katika Mungu na neema yake. Furaha katika Mungu ni nguvu ya maisha ya Kikristo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz