Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Zaburi hii imetungwa wakati mfalme Daudi alipomtoroka Sauli (habari hii inapatikana katika 1 Sam 22). Alijaa sana mawazo ya ukiwa, na aliona kwamba "makimbilio yamenipotea" (m.4). Alijisikia kuwa katika hali ya udhilifu kabisa. Ndipo akapata kuona kitu chenye maana sana: Mungu mwenyewe ndiye kimbilio lake (m.5,Bwana, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu, Fungu langu katika nchi ya walio hai)! Alipata uhakika kwamba Mungu anajua hali yake, na yuko tayari kumsaidia anapomlilia na kumtegemea. Mungu anajua shida yako pia, na ujue kabisa kwamba yeye ndiye kimbilio lako katika matatizo madogo na makubwa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz