Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 05/2020

SIKU 10 YA 31

Ayubu anabainisha hali ya watu wasio wa Mungu. Madhara ya kutokuwa na imani hai yako bayana. Huenda wanafanikiwa, lakini hata hapo hakuna kutosheka. Wanakabiliwa na hali inayotisha: Kuna kifo kisichoombolezwa (ling. Yer 15:2, Hapo watakapokuambia, Tutoke, tuende wapi? Utawaambia, Bwana asema hivi, Walioandikiwa kufa, watakwenda kufa; au kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; au kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa, au kutekwa nyara, watakuwa mateka). Uchumi wao hauaminiki, hutoweka kwa usiku mmoja (m.19,Hujilaza hali ni tajiri, lakini ndio mwisho; Hufunua macho yake, naye hayuko). Mwisho wa wasio haki ni kutoweshwa kwa kupoteza uhai. Hakuna Mungu wa kuwahurumia (m.21-22, Upepo wa mashariki humchukua, naye huondoka; Na kumkumba atoke mahali pake.Kwani Mungu atamtupia asimhurumie). Tunafanyaje tukishuhudia mwisho huu kwao? Kama ilivyoandikwa katika m.23? Tafakari mstari huu, Watu watampigia makofi, Na kumzomea atoke mahali pake.

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 05/2020

Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz