Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Ayubu anaitazama historia ya maisha yake aliyoishi hapo zamani. Haitazami tu, bali anaitafakari kwa kina. Anakumbuka ulinzi wa Mungu, na jinsi ushauri wake wa kirafiki ulivyompa mwangaza na kumfanya Ayubu kuwa msiri wa Mungu (m.4,Kama nilivyokuwa katika siku zangu za kukomaa, Hapo siri ya Mungu ilipokuwa hemani mwangu). Anakosa sana familia yake (m.5, Wakati Mwenyezi alipokuwa akali pamoja nami, Nao watoto wangu walipokuwa wakinizunguka). Zilikuwa nyakati za fahari zenye kuheshimiwa na kuogopwa. Ayubu anatamani hali hiyo tena, lakini kwa sasa haipo. Ulinzi, nuru, urafiki wa Mungu, watoto, maziwa, heshima - je, kipi kina maana zaidi kwako? Tafakari!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz