Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Fungu hili ni mwendelezo wa sehemu iliyotangulia (29:1-10). Ayubu anajipambanua. Anajitafakarisha juu ya matendo mema na upendo aliyowezeshwa kuyatenda kabla hajapata majaribu. Nyakati hizo alikuwa kituo cha faraja na kimbilio la wahitaji wa aina nyingi. Na wasio haki hawakujivuna kwake. Lakini hapo je, Ayubu alianza kujifurahia na kujisikia kana kwamba mkubwa ndiye yeye kuliko Mungu (m.18, Ndipo niliposema, Nitakufa ndani ya kioto changu, Nami nitaziongeza siku zangu kama mchanga. M.25, Niliwachagulia njia, nikakaa kama mkuu wao. Nikakaa kama mfalme katika jeshi la askari, Mfano wa awafarijiye hao waombolezao)? Jipime kwa habari za Ayubu. Je, unafurahia kutenda mema? Na una furaha kwa sababu gani?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz