Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Kama ilivyokuwa katika 16:12-13 Ayubu anataja matokeo ya majaribu yanayomkabili. Nafsi inamwagika, ameshikwa na dhiki, ana maumivu, anaugua na kifo kinakaribia. Hana thamani, utu wake umefananishwa na mnyama (m.29, Mimi ni ndugu yao mbwa-mwitu, Ni mwenzao mbuni). Wengi wangesema hiyo ni kazi ya shetani. Lakini Ayubu akisema, Yeye amenibwaga topeni (m.19), anamaanisha Mungu! Anahisi ukali wa Mungu. Na ingawa kilio chake ni kama vile hakisikiwi, Ayubu anaendelea kunyosha mkono kwa Mungu(m.24,Je! Mtu katika kuanguka kwake hanyoshi mkono? Na kulilia msaada katika msiba wake?)! Je, unafanyaje katika majaribu yako?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz