Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Kile unachokiamini, kukitegemea na kutarajia kitakuletea mema yote, ndicho Mungu wako. Basi, nini au nani amekuwa Mungu katika maisha ya Ayubu? Je, ni dhahabu yake, yaani, mali? Au ameabudu jua na nyota? (m.26-27,Kama nililitazama jua lilipoangaza, Au mwezi ukiendelea katika kung'aa;Na moyo wangu umeshawishwa kwa siri, Na midomo yangu imeubusu mkono wangu(wakati ule ilikuwa kawaida kubusu sanamu)). Hiyo ni mifano ya kushangilia na kusifia matunda badala ya mti uliozaa hayo. Wengi wamefanya hivyo (taz. k.mf. Zab 52:7,Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa nguvu zake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kujifanya hodari kwa madhara yake.Na Eze 8:16,Akanileta mpaka ua wa ndani wa nyumba ya Bwana, na tazama, mlangoni pa hekalu la Bwana, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwako watu kama ishirini na watano, wamelipa kisogo hekalu la Bwana, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki, nao wanaliabudu jua, kwa kuuelekea upande wa mashariki). Lakini Ayubu hafanyi hivyo. Ibada yoyote haipaswi kufanyika kwa ajili ya viumbe, bali hufanywa kwa Aliyeviumba.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz