Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Tafakari inayojidhihirisha kwa wazi katika aya hizi ni ya nadra sana kufanywa na watu. Ayubu anaorodhesha mambo ambayo kama yangefanywa naye, yangemwondolea tabia ya unyofu mbele za Mungu. Matendo ambayo yangesababisha hali hiyo, ni pamoja na 1) kunyanyasa mtumishi na wengine katika himaya yake. Kutenda hivyo kungekuwa kupuuza thamani ya mtu ambaye asili yake ni moja naye (m.15,Je! Huyo aliyenifanya mimi ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye? Si yeye mmoja aliyetufinyanga tumboni?). 2) Kutosaidia wahitaji. (Ukipenda, unaweza kulinganisha na Mt 25:31-42; tabia inayooneshwa hapa ni ile inayotajwa katika Zab 119:12, Ee Bwana, umehimidiwa, Unifundishe amri zako).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz