Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 05/2020

SIKU 17 YA 31

Mtu ateswaye anapokuwa na haki, mateso yake hugeuzwa kuwa ni ushuhuda wa uadilifu. Ayubu anajishuhudia juu ya maisha yake, kuwa mwenyewe haoni hatia yoyote, na hajaficha kitu. Hali yake yote ipo wazi mbele za Mungu. Lakini badala ya kujitetea hivyo, anampa Mungu nafasi yake ya kuwa mwamuzi wake mwenye haki. Kama kuna uovu, basi huo upimwe na Mungu mwenyewe (ling. m.4-6 na Mit 16:2: Je! Yeye hazioni njia zangu, Na kuzihesabu hatua zangu zote? Kwamba nimetembea katika ubatili, Na mguu wangu umeukimbilia udanganyifu;(Na nipimwe katika mizani iliyo sawasawa, Ili Mungu aujue uelekevu wangu). – Ling.: Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali Bwana huzipima roho za watu). Kukubali kupimwa ni alama ya uadilifu. Badala ya kujitetea tumwachie mwamuzi, tukimkabidhi njia yetu.

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 05/2020

Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz