Soma Biblia Kila Siku 05/2020Mfano
Maadui wanaitumia hali ya mwenye haki kama silaha yao. Hali yake ya awali iliwafanya wajizuie (Ayubu anadokeza hiyo akisema,Hawajizuii tena mbele yangu; m.11b), lakini sasa katika hali yake ya unyonge wanamletea mzaha. Ingawa hali ya wanaomdharau ni dhaifu (Ayubu anaifafanua katika m.2-8), amekuwa wimbo wa kicheko kwao. Wamemtenga na kumtendea kama mtu asiye na ulinzi. Mlinzi wa Ayubu ndiye Mungu, lakini sasa haonekani kwake tena. Basi, kwa wasio wema Ayubu ni mtu aliyeshindwa maisha. Wewe unamwonaje? Pima pia kama Ayubu anajihurumia kwa sababu tu ya kukosa heshima na mafanikio.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 05/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Ayubu, Zaburi na 1 Yohana. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz