Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

MWANGA Kuvutiwa Maishani Na Mwanga Ajabu Wa MunguMfano

MWANGA  Kuvutiwa Maishani Na Mwanga Ajabu Wa Mungu

SIKU 1 YA 5

Aina wengi wa kasa wa baharini wako katika hali ya hatari. Hii si kwa sababu ya wanyama wanowala, binadamu, ama kuzorota kwa mazingira; ila ni kwa sababu ya mwangaza usio wa kiasili unaopatikana kwenye ukingo wa bahari.

Mungu aliwaumba kasa wa baharini ili wawe wanazaliwa wakati wa mwezi mpevu. Kasa wanapoangua, mwangaza wa mwezi huwaongoza katika makaazi yao ya kiasili – baharini. Maisha ya kasa wa baharini yamo majini.

Watafiti walishangaa kupata kasa wachanga wakiwa wamekufa kwenye mwisho wa vinjia vya zigizagi vilivyokuwa katikati ya njia iliyo angaziwa na mwezi na zile za mwangaza wa bandia zilizotoka kwa nyumba za pwani, taa, na trafiki. Usumbufu kutokana na ile miangaza bandia ndio ulielekeza hao kasa kwenye vifo vyao.

Mwangaza Masomo ya Biblia ya Siku Tano yatakuvutia kwenye mnato wa mwangaza wa Yesu. “Mimi ndio mwangaza wa dunia…mwangaza inaoelekeza kwenye uhai” (Yohana 8:12). Pia yatakuvutia kwa Neno Lake – “Neno Langu ni mwangaza miguuini pako na mwangaza kwa njia yako” (Zaburi 119:105) na pia kukuwezesha kuwa mwangaza wa Kristo kwa ulimwengu wa giza “Nyinyi ni nuru ya dunia … ng’aeni kwa wote waone” (Mathayo 5:14).

Kila siku unaposoma, angazia, na utekeleze Neno la Mungu kwa maisha yako, utakuwa na uwezo zaidi wa kutambua miangaza bandia ya adui, bakia kwa njia iliyo angaziwa na Mungu, na ung’ae kwa mwangaza mkali kwa ajili ya Kristo, jamaa yako na jamii. 

Kila siku: soma maandiko, omba ili ufahamu na ujibu maswali.

Kulingana na maandiko haya, unaweza ukatoa maoni gani kuhusu Yesu Kristo? Ni mambo gani uliyojifunza kulingana na matendo ya Yesu Kristo?


Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

MWANGA  Kuvutiwa Maishani Na Mwanga Ajabu Wa Mungu

Kila siku unaposoma, angazia, na utekeleze Neno la Mungu kwa maisha yako, utakuwa na uwezo zaidi wa kutambua miangaza bandia ya adui, bakia kwa njia iliyo angaziwa na Mungu, na ung’ae kwa mwangaza mkali kwa ajili ya Kristo, jamaa yako na jamii.

More

Tunapenda hushukuru NBS2GO na Rebecca Davie kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://nbs2go.com/index.php/swahili/