Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano
Ingawa kanisa la Korintho lilikuwa na utajiri wa karama na viongozi wa kiroho (katika 8:7 Paulo anaandika kuwa wana wingi wa mambo yote; imani, na usemi, na elimu, na bidii yote) lilikuwa katika hatari ya kuanguka dhambini kwa sababu ya mafarakano. Mjumbe wa Neno la Mungu (Paulo) analikanya kanisa hili ili lijiepushe na tabia ya wasiomwamini Yesu Kristo. Hata kama maisha ya Wakorintho yalizingirwa na dhambi, Wakristo watembee nuruni mwa Kristo. Wakati huu wa soko huria, Wakristo tujihadhari tusiishi kihuria na kiholela. Bali tuongozwe na Injili ya Kristo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz