Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

SIKU 15 YA 31

Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi (m.1). Ndiye Mungu tunayemwamini: Muumba wa mbingu na nchi! Tusisahau kwamba Mungu ni mkubwa, na sisi ni vumbi tu. Mwanadamu akiwa na kiburi mbele ya Mungu ni ujinga. Ni kama nyenyere mdogo anayekuuma mguuni, hawezi kukufanyia lolote! Mungu aonapo ujinga huu, hucheka. Mbona mataifa wanafanya ghasia, Na makabila wanatafakari ubatili?Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya Bwana, Na juu ya masihi wake.Na tuvipasue vifungo vyao, Na kuzitupia mbali nasi kamba zao.Yeye aketiye mbinguni anacheka, Bwana anawafanyia dhihaka.Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake, Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake.Nami nimemweka mfalme wangu Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu(Zab 2:1-6). Sisi wanadamu tunapotengeneza kitu, k.m. baisikeli, twatumia vifaa. Ila Mungu alipoumba hapakuwa na kifaa cho chote. Ni utupu tu! Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri(Ebr 11:3).

Andiko

siku 14siku 16

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz