Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano
Siku ya sabaMungu akapumzika baada ya kuimaliza kazi yake yote ya uumbaji. Kutoka katika utupu Mungu aliumba vitu hivi vyote kwa nguvu ya NENO lake. Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika(Yn 1:1-3). Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa (m.3). Kwa hiyo binadamu hutakiwa vilevile kupumzika siku ya saba (Jumapili) baada ya kufanya kazi siku sita, maana ameumbwa kwa mfano wa Mungu (1:26-27). Kufanya kazi ni jambo muhimu. Na kupumzika pia ni jambo muhimu. Lakini kila jambo kwa wakati wake! Hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.Maana twasikia kwamba wako watu kwenu waendao bila utaratibu, hawana shughuli zao wenyewe, lakini wanajishughulisha na mambo ya wengine.Basi twawaagiza hao, na kuwaonya katika Bwana Yesu Kristo, watende kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.Lakini ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema.Na ikiwa mtu awaye yote halishiki neno letu la waraka huu, jihadharini na mtu huyo, wala msizungumze naye, apate kutahayari;lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu(2 The 3:10-15).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz