Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano
Nimepata mtoto mwanamume kwa BWANA(m.1). Hawa alitambua kwamba ni kwa nguvu ya Mungu na kwa upendo wake amepata mtoto. Huenda alifikiri kwamba Mungu tayari ameshatimiza ahadi yake, kwamba huyu mtoto ni uzao utakaomshinda nyoka (3:15, Nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino)! Kwa vyo vyote maneno haya yanatuonyesha kwamba Adamu na Hawa wamethibitika katika imani kwamba Mungu bado anawapenda! Lakini Kaini, mtoto wao wa kwanza, hakuwa na imani iliyokubalika mbele ya Mungu (m.3-5). Linganisha na ilivyoandikwa kuhusu Habili katika Ebr 11:4, Kwa imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kaini; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo, ijapokuwa amekufa, angali akinena.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz