Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano
Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa(m.24). Wengine wote katika ukoo wa Sethi wakafa (5:3-31). Ila Henoko hakufa, bali alichukuliwa na Mungu moja kwa moja Mbinguni, kama nabii Eliya. Kuhusu Henoko imeandikwa: Kwa imani Henoko alihamishwa, asije akaona mauti, wala hakuonekana, kwa sababu Mungu alimhamisha; maana kabla ya kuhamishwa alikuwa ameshuhudiwa kwamba amempendeza Mungu(Ebr 11:5). Kuhusu Eliya imeandikwa: Ikawa, Eliya na Elisha walipokuwa wakiendelea mbele na kuongea, tazama! Kukatokea gari la moto, na farasi wa moto, likawatenga wale wawili; naye Eliya akapanda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli. Naye Elisha akaona, akalia, Baba yangu, baba yangu, gari la Israeli na wapanda farasi wake! Asimwone tena kabisa (2 Fal 2:11-12). Henoko alipotwaliwa, wengi wa ukoo wake walikuwa bado hai. Bila shaka tukio hilo lilikuwa mwujiza mkubwa kwao! Ushuhuda wa Henoko ulikuwa wa pekee (m.22). Mtoto wake aliishi kuliko mtu yeyote aliyewahi kuishi, miaka 969 (m.27)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz