Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano
Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Utawanyiko, wakaao hali ya ugeni(m.1). Hao aliowaandikia mtume Petro walikaa sehemu mbalimbali (utawanyiko) katika eneo liitwalo Uturuki siku hizi. Walikuwa katika hali ya ugeni, maana ni wenyeji wa mbinguni (m.4: tupate na urithi usioharibika … uliotunzwa mbinguni). Walikuwa na sifa gani? Wamezaliwa mara ya pili, wametakaswa na Roho, wamenyunyiziwa damu ya Yesu Kristo, wametii (m.2-3: Mungu Baba alitangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kununyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu)! Hizi ni sifa zako pia? Barua hii ina mambo makuu 3: Tumaini(m.3-5), mateso(m.6-7) na ushahidiwa Wakristo!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz