Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano
Kwa mara ya kwanza damu ya mtu ilimwagika hapa duniani (m.9-10). Na ghadhabu ya Mungu ilikuwa kali sana (m.11-15). Kwa Kaini tunaona ukweli wa maneno ya Yakobo: Ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti. (Mengine ya hapo Yak 1:12-16 yanasema:Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike). Kwa Kaini chanzo chake kilikuwa hasira (m.5-6). Alipomwona Habili akikubalika mbele ya Bwana tofauti na yeye mwenyewe, akamwonea wivu badala ya kujuta na kutubu. Hasira ikazidi kukua moyoni mwake. Kisha ikakomaa (m.7-8)! Heri utubu dhambi zako leo. Usichelewe! Kumbuka ilivyoandikwa katika 1 Yoh 1:7-9:Tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz