Soma Biblia Kila Siku 10/2020Mfano
Siku ya nneMungu akaumba mianga, yaani jua, mwezi na nyota; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka(m.14). Ndivyo ilivyo hata leo. K.m. mwaka mmoja ni muda unaotumika na dunia kulizungukia jua (siku 365). Na siku moja ni kuanzia jua kucha mpaka litakapokucha tena mara nyingine. Na muda wa Waislamu kusherekea Ramadani na Wakristo kusherekea Pasaka unategemea mwenendo wa mwezi. Siku ya tanoMungu akaumba samaki na viumbe vingine baharini. Pia aliumba ndege warukao angani.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz