Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano
![Soma Biblia Kila Siku 11/2020](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F22531%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Bwana Yesu atakasa hekalu. Kwa tendo hilo, twaona kama kwa njia ya mfano kazi yake ya kutakasa mioyo ambayo ni hekalu la Roho Mtakatifu. Akemea uovu, na kutangaza utakatifu unaotarajiwa kwa waitwao kuwa wake. Awapa vipofu nuru kuonyesha awezavyo kufumbua watu macho ya rohoni, wamfahamu yeye na mapenzi yake. Awatia nguvu wasiojiweza kwa jinsi ileile atutiavyo nguvu na uweza kumtumikia. Na kama hatumzalii matunda atangaza hukumu (Yn 15:16, Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni). Mwisho, afundisha wanafunzi uweza ule atakaowavika wote watakaomwamini (Yn 14:12, Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku 11/2020](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F22531%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz