Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano
![Soma Biblia Kila Siku 11/2020](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F22531%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Wakuu wa dini waliudhiwa na tendo la Yesu kuingia ndani ya hekalu, kupindua meza zao waliokuwa wakiuza na kununua hapo, na kuwafukuza (m.12). Kwa tendo hilo, Yesu aliwapa fundisho na nafasi ili watambue dhambi zao, na waone jinsi wasivyotumika ipasavyo nyumbani mwa Mungu. Hata hivyo, hawa watumishi katika hekalu la Mungu hawakuona haja ya kutubu. Matokeo yake ni nini? Ni watoza ushuru na makahaba kutangulia mbele ya makuhani kuingia katika ufalme wa mbingu! Hali kama hii iko kwa Wakristo waishio katika mazoea ya kidini tu bila kutubu kweli.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku 11/2020](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapistaging.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans-staging%2F22531%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz