Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 12/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

SIKU 20 YA 31

Roho ya kuasi imekuwapo tangu alipoishi Paulo (m.7, Ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi), lakini bado yule mwovu hajafunuliwa (m.8, Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi), maana bado si wakati wake (m.6, Lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake). Yaani ni Mungu anayemzuia. Lizuialoau azuiaye(m.6-7), huenda maana yake ni jamii iliyojengwa juu ya haki, watu kujali amri za Mungu, au ushirika wa waumini. Ingawa yule asi atakuja kwa uwezo wote wa Shetani (m.9, Yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo), hatamweza Yesu, huyu atakapofunuliwa (m.8, Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwapo kwake). Angalia kwamba kutokea kwa mpinga Kristo ni mwanzo wa hukumu ya Mungu juu ya wasioiamini kweli ya Injili (m.10-12,Kuja kwake ni … katika madanganyo yote ya udhalimu kwa hao wanaopotea; kwa sababu hawakukubali kuipenda ile kweli, wapate kuokolewa. Kwa hiyo Mungu awaletea nguvu ya upotevu, wauamini uongo; ili wahukumiwe wote ambao hawakuiamini kweli, bali walikuwa wakijifurahisha katika udhalimu). Lakini waumini wataokolewa (2:13, Mungu amewachagua tangu mwanzo mpate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli).

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 12/2020

Soma Biblia Kila Siku 12/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wathesalonike, Mathayo na Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz