Soma Biblia Kila Siku Februari 2021Mfano
Somo la leo latufundisha mambo manne muhimu: 1. Dhambi za kila mtu, za kila kijiji, za kila mji na za kila taifa hapa duniani zajulikana kwa Mungu (m.20-21,Bwana akasema, … kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana.Alijua kwa kuwa kilio kimemjia)! 2. Mungu ni Mtakatifu. Dhambi zinamsikitisha na kumchukiza (ling. m.20-21 na malaika wanalosema katika 19:13, Tutapaharibu sisi mahali hapa, kwa kuwa kilio chake kimezidi mbele za Bwana; naye Bwana ametupeleka tupaharibu)! 3. Mungu ndiye atakayewahukumu wanadamu wote. Katika m.25 hukumu ilikuja juu ya Sodoma na Gomora: Mungu akaangusha miji hiyo na Bonde lote, na wote waliokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea katika nchi ile. Katika Ebr 4:13 na Ufu 20:11-15 wahusika ni sisi sote: Hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake [Mungu], lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu. - Nikawaona wafu, wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa na matendo yao.Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto.Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.Mtu, hata akifanya nini, hawezi kuepukana na hukumu ya Mungu siku ya mwisho. 4. Mji ukiwa na watu wa Mungu ndani yake ni baraka kwa huu mji (m.26, Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.Katika m.32 idadi ni kumi tu)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mwanzo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz