Soma Biblia Kila Siku Machi 2021Mfano
Kuna Wakristo waliokomaa kiimani na wengine walio wadhaifu na wachanga wa imani hiyo. K.mf. baadhi ya Wakristo wa Korintho waliona nyama iliyouzwa sokoni bado ni vyakula vilivyotambikiwa sanamu. Wachanga kama hao wanahitaji kuongozwa kama watoto wadogo bila kukwazwa kwa namna yoyote ile. Maisha yako yawe mfano ufaao kuigwa na hao walio wachanga wa imani. Angalia usijivunie ujuzi na uimara wako, usije ukaangamiza wengine. Badala yake, uwajibike katika kuwawezesha wanyonge hawa wamkaribie na kumwendea Mwokozi wao.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Machi 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi tembelea: http://www.somabiblia.or.tz